KABUDI ATOA SABABU TANZANIA KUTOHUDHURIA MIKUTANO YA EAC, SADC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi ametoa sababu za Tanzania kutoshiriki kwenye mikutano ya kikanda ukiwemo mkutano wa Korido ya Kaskazini wa Jumuiya ya Afrika  Mashariki unaohusisha nchi nne pamoja na mkutano wa SACU uliotishwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.


Profesa Kabudi alitoa ufafanuzi huo jana Mei 13,2020 Bungeni Mjini Dodoma 
Profesa Kabudi alianza kwa kuelezea mkutano uliohusisha nchi nne ambazo zinaunda Korido ya Kaskazini ambapo alisisitiza mkutano huo haukuwa unaihusu Tanzania ingawa ilikuwa na taarifa za kufanyika kwake.

"Mkutano ambao umefanyika ni wa Korido ya Kaskazini na walitutaarifu na tulijua, kwanini walitutaarifu lakini kwanini tuhudhurie mkutano wa Korido ya kaskazini? Ni wa kwao , ule haukuwa mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

"Na sitaki kurudia aliyoyasema Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka 2012, hayo yamepita tusiruhusu maadui zetu kutaka kuitingisha Jumuiya hii ya Afrika Mashariki. Wana yao na sisi tusiwe sehemu ya hayo, ndwele si sifa lakini Tanzania haijawahi kuacha kusimamia maslahi yake pamoja na udogo wa nchi hii kiuchumi.

"Nchi hii(Tanzania) imefanya mambo makubwa sana kwa hiyo nataka kuwahakikishia mkutano ule wa zile nchi nne ulikuwa ni mkutano wa majadiliano wa Korido ya kaskanini,lakini sisi na Rwanda tumekuwa na centre Corido , ndio maana sisi na Burundi hatukwenda, kwasababu Burundi ni Centre Corido.Kwanza utafanyikaje bila sisi kualikwa.Kwanza nilitaka hilo lieleweke na watu wasikuze,"alisema Profesa Kabudi wakati anatoa ufafanuzi.
Kuhusu mkutano ulioitishwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Profesa Kabudi alisema kuwa Rais huyo hakuitisha mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC),kwani mikutano ya SADC inaitishwa na Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo kwa kushiriana na Mwenyekiti .

Alisema kuwa mkutano uliotishwa na Rais Ramaphosa ulikuwa ni mkutano wa nchi ambazo ni majirani wa Afrika Kusini(SACU)ambao wengi wao wako SACU ukiondoa Zimbabwe ingawa inapakaa na Afrika kusini, Msumbuji na Angola na ndio maana nchi nane hazikuhudhururia.

Profesa Kabudi alizitaja nchi ambazo hazikuhudhuria mkutano huo wa SACU ni Tanzania, Zambia, Malawi,Madagasca, Mauritius, Comoro na DRC


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527