IGP SIRRO AWATAKA WANAOACHIWA KWA MSAMAHA WA RAIS KUFUATA SHERIA ZA NCHI


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amewataka baadhi ya wananchi ambao ni washtakiwa au wafungwa wanaopata msamaha wa Rais kutoka gerezani, kuacha kujiingiza katika matukio ya uhalifu jambo ambalo nikinyume na sheria za nchi.

IGP Sirro amesema hayo akiwa kwenye ziara ya ukaguzi mkoani Singida ambapo alizungumza na Polisi Kata waliopo kwenye mkoa huo na kuwataka kuendelea kushirikiana na wananchi katika mapambano dhidi ya uhalifu ikiwa pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuacha kujiingiza kwenye matukio ya uhalifu hususan wa kutumia silaha za moto.

Aidha, IGP Sirro amesema kuwa, wenyeviti wa kamati za Ulinzi na usalama za wilaya na mikoa kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi na kwamba hadi kufikia sasa hali ya usalama nchini imeendelea kuwa shwari.

Naye kamanda wa Polisi mkoa wa Singida Sweetbert Njewike amesema kuwa, hali ya usalama katika mkoa huo inaendelea kuwa shwari na kwamba matukio ya uhalifu yamepungua kutokana na ushirikiano mkubwa unaotolewa na wananchi pamoja na wadau wengine.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527