Picha : MBUNGE AZZA HILAL AKABIDHI KADI ZA BIMA YA AFYA ALIZOWAKATIA WAZEE KITUO CHA BUSANDA | MALUNDE 1 BLOG

Friday, May 8, 2020

Picha : MBUNGE AZZA HILAL AKABIDHI KADI ZA BIMA YA AFYA ALIZOWAKATIA WAZEE KITUO CHA BUSANDA

  Malunde       Friday, May 8, 2020
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad  (CCM) amekabidhi kadi za Bima ya afya iliyoboreshwa (ICHF) alizowakatia wazee 17 waliopo  kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ili wapate huduma za afya bila usumbufu.

Mhe. Azza amekabidhi kadi hizo za bima ya afya leo Ijumaa Mei 8,2020 alizoahidi kuwalipia alipofika katika kituo hicho Oktoba 5,2019 akiwa ameambatana Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kusherehekea Siku ya Wazee Duniani na kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula na magodoro. SOMA<<Soma Hapa>>
Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,
Mhe. Azza Hilal Hamad  (CCM) amkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kadi za Bima ya afya iliyoboreshwa (ICHF) alizowakatia wazee 17 wanaolelewa kwenye kituo cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ili wapate huduma za afya bila usumbufu. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiangalia kadi za bima ya afya kwa ajili ya wazee 17 waliopo katika kituo cha Busanda.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikabidhi bima za afya kwa wawakilishi wa wazee waliopo katika kituo cha Busanda zilizotolewa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad  (CCM).
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikabidhi bima za afya kwa wawakilishi wa wazee waliopo katika kituo cha Busanda zilizotolewa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad  (CCM).
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikabidhi Paroko wa Parokia ya Busanda,Padri Josephat Mahalubima za afya 17 zilizotolewa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad  (CCM) ili akawakabidhi wazee waliopo katika kituo cha Busanda.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post