Picha : DC MBONEKO AONGOZA WADAU KUSHEREHEKEA SIKU YA WAZEE KWA KUTOA MSAADA WA MAHITAJI KITUO CHA WAZEE BUSANDA


Wadau wa Maendeleo wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko wamesherehekea Siku ya Wazee Duniani kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 2.5 kwa ajili ya wazee wanaolelewa katika kituo cha Busanda kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.Wadau hao wamefika katika kituo hicho leo Jumamosi Oktoba 5,2019 kusherehekea Siku ya Wazee Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Oktoba 1.Akizungumza katika kituo kinachohudumia kaya 20 za wazee akiwa ameongozana na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM),Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta amesema wameamua kusherekea siku ya wazee duniani katika kituo hicho kwa kuwapatia mahitaji muhimu yanayotakiwa ili kuwapunguzia changamoto zinazowakabili wazee hao.

Mboneko alivitaja vitu vilivyotolewa na wadau kuwa ni magodoro 20,shuka 40,vyandarua 20,mchele kilo 200,sukari kilo 50,unga wa sembe kilo 225,maharage kilo 20,sabuni za miche boksi moja, sabuni ya unga kilo 15,mafuta ya kupaka katoni 2,mafuta ya kupikia lita 20,dagaa debe 2 ,dawa za meno katoni mbili,viberiti katoni 2,chumvi katoni 1,juisi katoni 2 na nyanya debe moja.

Mkuu huyo wa wilaya amewashukuru wadau waliojitokeza kutoa msaada wa vitu hivyo vilivyogharimu jumla ya shilingi milioni mbili,laki tano na elfu ambao ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Superdoll Seif Said Seif aliyetoa msaada wa magodoro 20,vyandarua na shuka vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni moja na laki nne.

"Kwa namna ya pekee niwashukuru wadau walioguswa kutoa mchango kusaidia wazee wetu hawa.Wadau hawa ni pamoja Mkurugenzi wa Makampuni ya Superdoll,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko,Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal,Watumishi na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Hoja Mahiba na watumishi wa benki ya NBC",alisema Mboneko.

"Wadau wengine ni Kwaya ya Malaika Wakuu Kanisa Katoliki Ngokolo,Familia ya Richard Male,Familia ya mama Shine,Mama Mihambo na marafiki zake,Gilitu,Said Makilagi (Musoma Food),Dada Scola na Lightness,waandishi wa habari na wadau wengine ambao sijawataja ambao kwa pamoja wamefanikisha kupatikana kwa mahitaji haya kwa ajili ya wazee wetu",aliongeza Mboneko.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kila mtu ni mzee mtarajiwa hivyo ni vyema tukawapenda na kuwapatia mahitaji wazee huku akisisitiza msaada huo ni kwa ajili ya walengwa tu hivyo kuwataka watu wenye uwezo wafanye kazi ili kujipatia mahitaji yao.

Kwa upande wake,Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad aliahidi kuwalipia Bima ya afya iliyoboreshwa (ICHF) wazee 11 waliopo katika kituo cha Busanda ili wapate huduma za afya bila usumbufu.

Mbunge huyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24 mwaka huu kwa kujitokeza kugombea na kuchagua viongozi wenye kusaidia jamii.
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza baada ya kuwasili katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakati wa hafla fupi ya kukabidhi mahitaji mbalimbali ya wazee katika kituo hicho. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM). Picha zote na Kadama Malunde na Marco Maduhu - Malunde 1 blog
Paroko wa Parokia ya Busanda,Padri Josephat Mahalu akimkaribisha Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakati wa hafla fupi ya kukabidhi mahitaji mbalimbali ya wazee katika kituo hicho. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Nganganulwa kilipo kituo hicho,George Charles akifuatiwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akielezea kuhusu msaada wa vitu mbalimbali pichani vilivyotolewa na wadau wa maendeleo kwa ajili ya kusaidia wazee wanaolelewa  katika kituo cha Busanda.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Kulia ni Paroko wa Parokia ya Busanda,Padri Josephat Mahalu. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Kituo cha Kulelea Wazee cha Busanda, Elias Shilanga akielezea kuhusu kituo cha Busanda. 
Sehemu ya vitu vilivyotolewa na wadau wa maendeleo kwa ajili ya wazee wanaolelewa katika kituo cha Busanda.
Wadau wakijiandaa kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya wazee katika kituo cha Busanda.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akikabidhi unga wa sembe bi Mary Barabara katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.Kila mzee alipokea msaada wa unga wa sembe,mchele,sukari,mafuta ya kupaka,mafuta ya kupikia,sabuni,godoro,shuka 2,vyandarua,maharage n.k
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akimkabidhi mafuta ya kupikia bi Mary Barabara katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akikabidhi godoro,shuka,chandarua kwa bibi (kulia).
Zoezi la kukabidhi godoro,shuka na chandarua likiendelea.
Bibi akifurahia baada ya kupokea mahitaji mbalimbali.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akikabidhi mafuta ya kupikia kwa bibi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akiendelea kugawa mafuta ya kupikia.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga akisaidiana na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kubeba mfuko wa nyanya wakati wa kugawa vitu mbalimbali vilivyotolewa na wadau wa maendeleo kwa ajili ya wazee katika kituo cha Busanda.
Zoezi la kuweka sabuni za kufulia kwenye mifuko ili kugawa kwa wazee likiendelea.
Zoezi la kuweka sabuni ya unga kwenye mifuko likiendelea.
Zoezi la kuweka sabuni ya unga kwenye mifuko likiendelea.
Mdau Said Nassoro akigawa sabuni ya unga.
Zoezi la kugawa sabuni likiendelea.
Mzee Zacharia Makaranga akiwashukuru wadau waliotoa msaada kwa wazee wanaolelewa katika kituo cha Busanda.
Bibi akishukuru kwa msaada uliotolewa na wadau.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akifurahia jambo na wazee wakati akigawa mchele,unga na mahitaji mengine.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad wakiagana na wazee katika kituo cha Busanda

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad wakiagana na wazee katika kituo cha Busanda.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akiagana na Paroko wa Parokia ya Busanda,Padri Josephat Mahalu  baada ya kukabidhi msaada uliotolewa na wadau wa maendeleo katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akiagana na Paroko wa Parokia ya Busanda,Padri Josephat Mahalu  baada ya kukabidhi msaada uliotolewa na wadau wa maendeleo katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post