Watu wengine 12 wamepatikana na virusi vya corona nchini Kenya ndani ya masaa 24 yaliyopita.
Sasa idadi ya watu walioambukizwa virusi hivyo nchini Kenya imefikia 355 tangu kisa cha kwanza kiripotiwe Machi 13 mwaka huu.
Taarifa hiyo imetolewa leo Jumapili, Aprili 26, na katibu msimamizi katika Wizara ya Afya Rashid Aman.
Aman amesema kuwa hakuna kifo zaidi kimeripotiwa kutokana na virusi hivyo na idadi ya waliofariki imesalia watu 14.
Watu 8 wamepona virusi hivyo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 106