WENYE VIRUSI VYA CORONA NCHINI KENYA WAFIKA 110...WAWILI ZAIDI WAFARIKI DUNIA


Idadi ya visa vya ugonjwa wa virusi vya corona nchini Kenya imefikia 110 baada ya visa vingine 29 kuthibitishwa.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari jijini Nairobi waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema kwamba watu wengine wawili wamepoteza maisha yao kutokana na maambukizi ya virusi hivyo.

Amesema kwamba idadi hiyo inaongeza idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo kufikia 3. Kagwe ameongezea kwamba wagonjwa waliofariki wanatoka miji ya Nairobi na Mombasa.

Waziri huyo pia amepiga marufuku usafiri wa Wakenya kuelekea katika maeneo ya mashambani akionya kwamba huenda wakapeleka maambukizi ya virusi hivyo katika maeneo hayo.


Amesema kwamba serikali imewapima watu 662 katika kipindi cha saa 24 ambapo takriban watu 29 wamepatikana na virusi hivyo.

Kagwe amesema kwamba wagonjwa 28 kati ya wale waliopatikana na virusi hivyo ni raia wa Kenya huku mmoja akiwa raia wa DR Congo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527