WATU 20,000 WAFARIKI KWA CORONA NCHINI MAREKANI


Washington, Watu 1,920 wamekufa nchini Marekani kutokana na virusi vya corona katika kipindi cha saa 24 zilizopita na kuifanya nchi hiyo kuwa ya kwanza duniani kwa idadi kubwa ya vifo vilivyosababishwa na ugonjwa wa COVID-19.

Taarifa iliyochapishwa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins imeonesha idadi ya vifo nchini Marekani imepindukia watu 20,000 ambayo ni kubwa ikilinganishwa na vifo 19,500 vilivyotokea nchini Italia.

Kulingana na takwimu zilizopo, taifa hilo pia linaongoza kwa visa vya maambukizi ya virusi vya corona na hadi sasa kuna idadi ya watu 527,111 waliothibitika kuambukizwa.

Wakati huo huo, idadi jumla ya maambukizi ya virusi vya corona duniani imepindukia watu milioni 1.7 leo, na virusi hivyo tayari vimesababsiha vifo vya zaidi ya watu 107,000 tangu vilipozuka kwa mara ya kwanza nchini China, Disemba iliyopita.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post