WATU 1,169 WAFARIKI KWA CORONA NCHINI MAREKANI NDANI YA MASAA 24.....MAAMBUKIZI DUNIANI SASA YAFIKA MILIONI 1


 Ugonjwa wa Covid-19 unaendelea kuathiri nchi mbalimbali duniani, huku maambukizi ya ugonjwa huo duniani yakifikia milioni moja, huku watu wakiendelea kufariki dunia kutokana na ugonjwa huo.

Wakati huo huo Marekani inaendelea kuripoti visa vingi vya maambukizi ya virusi vya Corona, ambapo vifo vya watu 1,169 vimeripotiwa ndani ya masaa 24.

Uchumi umeangamizwa na janga hilo, kama inavyoonyesha takwimu nyingine ambayo inatisha: katika wiki moja, Wamarekani milioni 6.6 wamepoteza kazi. Nusu ya watu duniani wamekwama kutokana na hatua ya kukaa nyumbani ambayo kwa baadhi ya nchi imekuwa kali.

Idadi ya visa vya maambukizi vilivyothibitishwa ulimwenguni inazidi milioni moja leo Ijumaa, huku watu 52,000 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa Covid-19, kulingana na takwimu zilizotolewa na shirika la habari la AFP.

Ulaya ndio bara lililoathiriwa zaidi, lakini Marekani inaelekea kuwa kitovu kipya cha janga hilo, ikiripoti robo ya visa vya maambukizi. Idadi hii labda ni ndogo, kwa sababu ya ukosefu wa uchunguzi wa kutosha.

Nchini Marekani, idadi ya vifo katika masaa 24 imeiweka nchi hiyo kuwa na rekodi kubwa zaidi: vifo 1,169, kulingana na ripoti ya Chuo Kikuu cha Marekani cha Johns Hopkins.

-RFI


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post