DC KAHAMA AAGIZA WACHEZA BAO NA KARATA NDANI YA MASOKO WAKAMATWE

SALVATORY NTANDU

Serikali Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga imesema itachukua hatua kali kwa baadhi ya wananchi wanaokaidi maelekezo ya Wizara ya afya Maendeleo ya jamii jinsia, wazee na watoto, wanaopenda kwenda kwenye masoko kucheza michezo ya bao, karata na madrafti ili kudhibiti mikusanyiko isiyokuwa na tija katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona.

Kauli hiyo imetolewa Machi 31 Mwaka huu na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Anamringi Macha wakati akizungumza na Mwandishi wa Habari wa Mpekuzi Blogs Ofisini kwake kuhusiana na hatua zinazoendelea kuchukuliwa na dhidi ya  ugonjwa huo.

“Tumebaini katika Masoko ya Kariakoo na Namanga CDT kunabaadhi ya wananchi wanaingia ndani kwa lengo la kucheza bao, karatana drafti sasa hawa tuwachukulia hatua za kisheria, tunaomba wananchi wanaoingia katika masoko yetu wawe ni wale wanaohiji huduma tuu na si vinginevyo,”alisema Macha.

Macha aliongeza kuwa kwa sasa Halmashauri ya Mji wa Kahama imeshaweka utaratibu maalum wa kuingia na kutoka  katika Masoko haya hivyo ni budi wananchi wakatii maelekezo ya kunawa mikono na sabuni bila kushurutishwa ili kujikinga na Ugonjwa huu ambao tayari umesharipotiwa kuwepo hapa nchini.

“Tulifanya  ziara wiki iliyopita  na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainab Telack katika Halmashauri tatu za Msalala,Mji kahama na Ushetu kuhimiza wafanyabiasha na wananchi wote kwa ujumla kuzingatia maelekezo ya Serikali juu ya kujikinga na ugonjwa huu na watakaobainika kwenda kinyume tutawachukulia hatua kali,”alisema Macha.

Kwa upande wake Hamaza Shabani Mfanyabiashara katika Soko kuu la Kariakoo Mjini Kahama alikiri kuwepo kwa watua wanaopenda kukaa katika sokoni hapo na kucheza michezo mbalilmbali ikiwemo kamari kwa kutumia karata licha ya serikali kuzuia mikusanyiko.

“Wapo vijana wanapenda kukaa kaa humu bila kuwa na shughuli maalumu na badala yake hujikuta wakicheza michezo ya karata na drafti na kusababiasha mikusanyiko isiyokuwa na tija tunashukuru kama serikali imeliona hili wazuieni kuingia humu ikiwezakana wekeni migambo kuwadhibiti,”alisema Shabani.

Monica Sweya ni Mfanyabiasha katika Soko la Namanga CDT katika Halamshauri ya Mji Kahama ameiomba serikali kuweka utaratibu wa wananchi kuingia katika masoko ili kuzui maambukizi ya Ugonjwa na unaosababishwa na virusi vya Corona.

“Naiomba  Halmashauri iweke walinzi ambao watawaelekeza wananchi kunawa mikono kabla ya kuingia sokoni kwa utaratibu malumu sambamba na kuwalazimisha  kutumia milango miwili kuingia na kutoka ili kudhibiti ugonjwa huo”,alisema Sweya.

Mpaka sasa Wizara ya afya maendeleo ya Jamii,jinsia wazee na watoto kupitia kwa waziri wake, Ummy Mwalimu imetangaza watu 19 nchini ndio waliothibitika kuwa na ungonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post