UNUNUZI WA TIKETI KUFANYIKA KWA NJIA YA MTANDAO ILI KUKABILIANA NA CORONA


Katika  kukabiliana na mambukizi ya virusi vya Corona katika vituo vya mabasi serikali imesema mfumo wa ukatishaji tiketi kwa njia ya mtandao utaanza hivi karibuni kwa mabasi yote yanayofanya safari zake mikoani.

Mbali na mabasi hayo, daladala pamoja na mabasi ya mwendokasi yanatarajiwa (Data center) ambapo mfumo huo utarahisisha huduma na kuondoa adha ya wapiga debe vituoni.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano , Mhandishi Isack Kamwele, wakati wa ukaguzi wa mifumo hiyo jana Dar es Salaam alisema hatua hiyo itafikiwa hivi karibuni ambapo kiu ya serikali ni kuona wananchi wananufaika kwa kuondoshewa adha ya usafiri.

Mhandisi Kamwelwe alisema serikali imefikia hatua ya mwisho ya kuanza kutumika kwa mfumo huo ambapo wananchi watatumia simu kukata tiketi za mabasi na hawatolazimika kutembelea vituoni jambo litakalowaepusha na wizi unaofanywa kupitia ulanguzi wa tiketi na wapiga debe.

“Nimeridhishwa na mfumo, huu ambao utasimamiwa na serikali kupitia kituo chetu cha Data center ukweli utasaidia sana wananchi wetu hususani wale wa chini ambao walikuwa wanaingia gharama kwenda katika vituoni kukata tiketi, tumefika wakati wa kuwa kisasa zaidi wapiga debe walikuwa wakiongeza gharama lakini wakati huu wa maambukizi ya corona ni muhimu kutafuta njia mbadala katika usafirishaji,”alisema.

Mhandisi Kamwele alisema, mfumo huo ameungahikia kwa muda mrefu hatimaye sasa unafika mwisho ambapo ameridhaka na uandaaji wa kimifumo kwakuwa taarifa zitatunzwa vizuri na kufanya kazi kwa ushirikishi wa wadau wa usafiri nchini.

“Hakuna sababu ya msafiri kutembea na pesa mkononi, hata wanaopandia njiani ni wakati wa kuwa na pesa kwenye simu, kwakuwa hatuna uhakika iwapo ugonjwa huu utaenea hadi kwenye noti ni lazima kuwa na njia nyingi za udhibiti,”alisema.

Alisema wamiliki wa mabasi walikuwa na maswali mengi wakati wa mchakato wa mfumo huo, wakihofia kupata hasara lakini ni wazi utendaji wake utanufaisha pande zote.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527