TRUMP AITUHUMU CHINA KWAMBA INAFANYA KILA MBINU ILI ASICHAGULIWE TENA KUWA RAIS WA MAREKANI


Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba China inampango wa kutumia kila njia ili kumfanya asichaguliwe  tena kwenye uchaguzi mkuu wa Urais unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.


Katika mahojiano yaliofanyika katika Ikulu ya Whitehouse na chombo cha habari cha Reuters, amesema kwamba China inakabiliwa na athari chungu nzima kutoka kwa Marekani kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Anasema China ilificha kuhusu ugonjwa wa Corona na hivyo kuufanya usambae dunia nzima na kuleta madhara makubwa. 

Hata hivyo, Trump yeye mwenyewe amekuwa akikosolewa vikali  kwa Jinsi anavyokabiliana na tatizo hilo.

Mlipuko wa virusi vya corona umeharibu uchumi wa Marekani ambao Trump alikuwa akitumia  kama kinga kujipigia debe ili kuchaguliwa tena katika uchaguzi wa mwezi Novemba mwaka huu.

"China inafanya kila mbinu za kutaka nishindwe katika uchaguzi ujao. Wanataka mpinzani wangu mkuu kutoka chama cha Democrat Joe Biden ndo ashinde uchaguzi wa mwezi Novemba."-Trump

Aidha, Trump amepinga vikali utafiti uliofanyika nchini humo na kutoa maoni kwamba mpinzani wake  Biden  ana asilimia kubwa za kuibuka  mshindi.

"Siamini kura hizo za maoni....Naamini  raia wa taifa hili ni watu werevu. Na sidhani kama watamchagua mtu ambaye hawezi kuwasaidia kutatua  changamoto zao''. -Trump


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527