TRUMP AIONYA INDIA KUHUSU KUSITISHA MAUZO YA HYDOXY-CHLOROQUINE....ASEMA ATALIPA KISASI


Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kulipiza kisasi dhidi ya India ikiwa nchi hiyo itapiga marufuku mauzo ya dawa aina ya Hydoxy-chloroquine. 

Trump amedai kwamba dawa hiyo inaweza kutibu maradhi ya homa ya mapafu yanayosababishwa na virusi vya corona. 

Hata hivyo India ambayo ni mzalishaji mkuu wa dawa hiyo duniani imepiga marufuku kuuzwa dawa hiyo nje.

 Rais Trump amesema amezungumza na waziri mkuu wa India Narendra Modi na kumwambia kuwa Marekani inapendelea kuzipata dawa ilizoagiza. 

Dawa hiyo ya Hydroxy-chloroquine inatumika kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa malaria. 

Hata hivyo sasa inafanyiwa majaribio kubainisha iwapo inaweza kutumika kutibu ugonjwa wa Covid -19 unaosababishwa na maambukizi wa virusi vya corona.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527