Tanzia : MCHUNGAJI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO GETRUDE RWAKATARE AFARIKI DUNIA

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) na Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto (Mikocheni B Assemblies of God ) Mchungaji Dkt.Getrude Rwakatare amefariki dunia Alfajiri ya leo Jumatatu Aprili 20,2020.

Kwa mujibu wa mtoto wake Muta Rwakatare amesema marehemu alikuwa akisumbuliwa na Presha.

"Ni bahati mbaya imetokea asubuhi ya leo saa 11 kasoro, alikuwa na matatizo ya moyo, jana tulimkimbiza Hospitali lakini bahati mbaya imetokea, tupo katika hatua ya kuangalia namna gani tutafanya ili tuweze kumpumzisha mama yetu", amesema Muta.

Mama Rwakatare alizaliwa Disemba 31, 1950, na hivyo amefariki akiwa na umri wa miaka 70.

Ikumbukwe kuwa Mama Rwakatare aliwahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Mvomero kuanzia mwaka 2008 hadi 2015, na baadaye mwaka 2017 aliapishwa na Spika wa Bunge Job Ndugai, kama Mbunge wa kuteuliwa na Rais wa kipindi hicho Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post