SERIKALI KUTOA VITABU MSINGI, SEKONDARI KWA MTANDAO BURE ILI WANAFUNZI WAJISOMEE WAKIWA NYUMBANI


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako amesema kwa sasa serikali inatoa huduma ya upatikanaji wa vitabu vyote kuanzia shule za msingi na sekondari kwenye maktaba bila malipo yeyote kwa njia ya mtandao.

“Tunatambua kwamba wanafunzi wapo nyumbani na wanahitaji kuendelea kupata elimu hata wakiwa nyumbani, tunayohuduma ya maktaba inayotolewa na Taasisi ya Elimu Tanzania ambayo kiutaratibu ili uweze kupata vitabu ilipaswa mtu kulipa, sasa serikali inatoa huduma ya upatikanaji wa vitabu vyote kuanzia shule za msingi na sekondari bila malipo yeyote,”amesema.

Amewataka wanafunzi kutumia muda wao kusoma vitabu ambavyo serikali imewapa fursa bila gharama yeyote badala ya kuzurura mitaani na kujiweka  kwenye hatari ya kupata maambukizi ya corona.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post