RAIS MAGUFULI ATIMIZA AHADI YAKE “MAAFISA TARAFA MWANZA WAKABIDHIWA USAFIRI”

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) akikabidhi ufunguo wa pikipiki kwa Mwenyekiti wa Maafisa Tarafa Mkoa Mwanza, Peter Michael (kushoto) kama ishara ya kukabidhi pikipiki 24 kwa Maafisa Tarafa wa Tarafa zote 24 za Mkoa Mwanza.


Mongella amekabidhi pikipiki hizo kwa niaba ya Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake (ahadi ya Rais Dkt. Magufuli) ya kutoa pikipiki kwa Maafisa Tarafa wote Tanzania aliyoitoa alipokutana na viongozi hao Juni 04, 2019 Ikulu jijini Dar es salaam.

Akizungumza baada ya kukabidhi pikipiki hizo, Mongella amewataka Maafisa Tarafa mkoani Mwanza kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa na si kuzifanyia biashara (bodaboda) huku wakisimamia ipasavyo maelekezo ya Serikali katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona (Covid- 19).

Na George Binagi-GB Pazzo, Mwanza
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akikabidhi pikipiki kwa Maafisa Tarafa Mkoa Mwanza.
Pikipiki hizo zitaondoa adha ya usafiri kwa Maafisa Tarafa na hivyo kutekeleza vyema wajibu wao wa kuwatumikia wananchi.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) akikabidhi kofia ngumu (helment) kwa mmoja wa Maafisa Tarafa Mkoa Mwanza.
"Tunamwahidi Rais Magufuli kuwa tutachapa kazi kwa bidii zaidi" Maafisa Tarafa Mkoa Mwanza.
Pikipiki zilizotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa Maafisa Tarafa Mkoa Mwanza.
Tazama video hapa chini


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post