MPANGAJI ANG'OLEWA PAA LA NYUMBA BAADA YA KUCHELEWA KULIPA KODI YA NYUMBA

Mwanaume aitwaye Jackson Ng’ang’a Mwangi, mwenye miaka 35 kutoka mtaa wa Kariobangi South, Nairobi nchini Kenya ameng’olewa paa la nyumba kwa kuchelewa kulipa kodi ya mwezi huu. 
Jackson Ng’ang’a Mwangi alisema mwanawe mmiliki wa nyumba hiyo alitekeleza kitendo hicho jana Jumatatu, Aprili 20, ilhali amekuwa akimlipa kodi ya KSh6,000 kila mwezi kwa miaka miwili bila kuchelewa. 

Mpangaji huyo anadai amekuwa akimlipa kodi ya KSh6,000 kila mwezi kwa miaka miwili bila kuchelewa na ameshindwa kulipa kodi ya nyumba kutokana na kudhorora kwa uchumi ambako kumechangiwa na janga la virusi vya Corona.

Mpangaji huyo ambaye amekodisha nyumba ya vyumba viwili, amesema kwamba alikuwa amemuomba mpangishaji huyo kumpa muda lakini alipokwenda kutafuta riziki alipigwa simu na jirani kufahamisha kuwa paa la nyumba limeng’olewa.

“Juzi nilimwambia kijana wa mwenye nyumba kwamba anipe muda nitafute pesa nitamlipa lakini akasisitiza kuwa sharti nimpe pesa hizo leo (Jumatatu) la sivyo nihame. Na leo asubuhi nilipoondokwa kwenda kutafuta riziki jirani alinipigia simu kwamba amekuja na kung’oa paa la nyumba,”

Mpangaji huyo anaendesha biashara ya kuuza kanda za nyimbo za injili katika mtaa wa Huruma, alisema ameshindwa kulipa kodi ya nyumba kutokana na kudhorora kwa uchumi ambako kumechangiwa na janga la virusi vya corona.

“Sijakataa kulipa, lakini biashara sio nzuri wakati huu kwa sababu wateja wangu wengi wameathirika na makali ya corona,” aliongezea Mpangaji huyo.

Mtoto wa mmliki wa nyumba hiyo aliyetambuliwa kama Mwash, amesema kuwa ni lazima Mwangi alipe kodi ya ama ahame.

“Huyu jamaa lazima alipe pesa. Mbona analalamika ilhali wapangaji wengine wamelipa. Kwani wao hutoa wapi pesa?” alisema Mwash. Mwangi aliandikisha taarifa kwa kituo cha polisi cha Kinyago katika mtaa wa Dandora Phase 1


Chanzo -TUKO SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527