MUSEVENI ATAKA WENYE NYUMBA WASIWAFUKUZE WAPANGAJI WAKATI HUU WA MLIPUKO WA CORONA


Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ametoa onyo kwa wapangaji nchini humo na kuwataka wasiwafukuze wapangaji wanaoshindwa kulipa kodi katika wakati huu ambapo nchi hiyo inakabiliana na janga la Corona.

Museveni amesema huu sio mwisho wa dunia na kwamba wenye nyumba wanapaswa kuwa wavumilivu na waelewa kwani janga hili litakapoisha, madeni yote yatalipwa

Pamoja na hayo, Rais Museveni pia amewaagiza Polisi nchini humo kuingilia kati pale wanapokuta mpangaji anafukuzwa

Wiki iliyopita Rais Museveni alitangaza amri ya kutotoka nje na kusalia nyumbani kwa siku 14 kuanzia 1.000 usiku hadi 12.00 asubuhi.

Pia, Rais Museveni alipiga marufuku watu kuendesha magari yao isipokuwa ya kusafirisha mizigo na kutokufunguliwa kwa maduka na kuruhusu biashara ya vyakula pekee.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527