Tanzia : MTANGAZAJI WA TBC MARIN HASSAN AFARIKI DUNIA


Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Marin Hassan Marin wa TBC amefariki dunia leo Aprili Mosi asubuhi katika Hospitali ya Jeshi Lugalo, jijini Dar es Salaam. 

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mkurugenzi wa TBC, Dkt. Ayub Rioba pamoja na wana familia.

Kabla ya kufanya kazi TBC Marin alifanya kazi Televisheni ya Zanzibar (TVZ) na ni miongoni mwa waandishi walionesha kipaji mapema wakati wakianza kazi ya uandishi wa habari, Marin pia ni katika waanzilishi wa kipindi cha Redio cha Mawio kilichokuwa zikikirushwa na Sauti ya Tanzania Zanzibar (STZ) ambacho kinaendelea hadi leo kwenye Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC).

Mwili wa Marehemu utapelekwa Zanzibar kwa mazishi.

R.I.P Marin

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527