MAREKANI WAANDAMANA KUPINGA MARUFUKU YA KUTOTOKA NJE KISA CORONA


Waandamanaji nchini Marekani wameingia mitaani katika majimbo kadhaa wakishinikiza magavana kufungua uchumi wa majimbo yao kwa kuondosha amri ya kutokutoka nje.


Marufuku hiyo ya kutokutoka nje imewekwa katika majimbo yote ya Marekani ili kudhibiti kusambaa kwa janga la virusi vya corona, hali iliyotikisa uchumi wa taifa hilo kubwa zaidi kiuchumi duniani.

Maaandamano yameripotiwa jana Jumapili katika majimbo ya Arizona, Colorado, Montana na Washington, huku mwendelezo wa maandamano hayo ukitarajiwa leo Jumatatu.

Hasira juu ya marufuku hizo imeongezeka nchini humo huku waandamanaji wakitaka masharti yalegezwe.

Rais wa Marekani Donald Trump ameonesha dalili za kukubaliana na maandamano hayo.

Kwa sasa, Marekani ndiyo kitovu cha janga la ugonjwa wa virusi vya corona duniani. Hata hivyo kuna dalili kuwa maambukizi yanafikia kileleni nchini humo na kasi ya maambukizi kuanza kushuka katika baadhi ya majimbo. 

-BBC


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527