KWA MARA YA KWANZA CHINA YASEMA HAIJAREKODI KIFO CHOCHOTE CHA CORONA NDANI YA MASAA 24


Serikali ya China imetangaza kwa mara ya kwanza kutokuwa na vifo vipya tangu virusi vya corona vilipoibuka mwishoni mwa mwaka 2019 ambapo Watu 3,331 wamefariki huku Wagonjwa wakiwa 81,740 na waliopona ni 77,167. 


 Kwa mujibu wa Tume ya Kitaifa ya Afya, hakujarekodiwa pia kisa chochote cha maambukizi ya ndani ya nchi katika mkoa wa Hubei na kote nchini humo. 

Viongozi nchini humo wameripoti visa 32 vipya vya virusi vya corona ila vyote ni kutoka kwa raia wa China walioingia kutoka nchi za nje. 

Tume hiyo ya afya pia imesema inaviangalia kwa karibu visa vingine 30 vipya vya watu wanaoshukiwa kuwa na virusi hivyo ila hawaonyeshi dalili zozote.

 Jumla ya visa zaidi ya elfu moja vya aina hiyo vimeripotiwa China na vinafuatiliwa kwa karibu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post