KOREA KUSINI KUCHUNGUZA MADAI YA MAREKANI KUWA RAIS WA KORA KASKAZIN KIM JONG UN ANA HALI MBAYA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, April 21, 2020

KOREA KUSINI KUCHUNGUZA MADAI YA MAREKANI KUWA RAIS WA KORA KASKAZIN KIM JONG UN ANA HALI MBAYA

  Malunde       Tuesday, April 21, 2020

Serikali ya Korea Kusini inaangalia undani wa taarifa zilizoripotiwa na Vyombo vya Habari vya Marekani kuwa Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un ana hali mbaya baada ya kufanyiwa upasuaji.

Maafisa wa Korea Kusini wamesema hawawezi kudhibitisha ripoti hiyo mara moja. 

CNN kimemnukuu Afisa wa Marekani ambaye alisema Kim yupo katika hali mbaya baada ya kufanya upasuaji ambao haukuwekwa wazi.

Kumekuwa na sintofahamu kuhusu afya ya Kim baada ya Kiongozi huyo kushindwa kuhudhuria hafla ya Kumbukumbu ya Marehemu babu yake, Kim Il Sun ambaye pia ni muasisi wa Taifa hilo wiki iliyopita.

Inaelezwa kuwa afya ya Kim Jong Un imezorota miezi ya hivi karibuni kutokana na uvutaji sigara, unene uliopitiliza na kufanya kazi kwa muda mrefu.

Alionekana kwa mara ya mwisho Aprili 11 ambapo aliongoza kikao na kisha kuelekea hospitali, chanzo kimoja kimesema kuwa Kim amekuwa akiugua tangu Agosti mwaka jana.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post