MWANAJESHI WA JWTZ AUAWA NA WANAODHANIWA KUWA VIBAKA...WATU WATANO MATATANI


 Kutokana na kuuawa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) usiku wa kuamkia juzi jumla ya watu watano wamekamatwa wakituhumiwa kuhusika na mauaji hayo.

Mwanajeshi huyo, Samwel Machugu (28) aliuawa na watu wanaodhaniwa vibaka wakati akienda nyumbani kwake baada ya kushiriki ulinzi shirikishi.

Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Komanya Kitwala amesema watuhumiwa waliokamatwa wanaendelea na mahojiano kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa kwa jalada lao kupelekwa ofisi ya Mkurugenzi Mashtaka (DPP).

Mwanajeshi Samwel Machugu aliagwa jana Jumanne Machi 31 na jioni kusafirishwa kwenda Tarime mkoani Mara kwa maziko.

Marehemu aliajiriwa mwaka 2015 na amefariki akiacha mtoto wa miezi sita na mke ambaye wameishi naye kwa miezi minne tangu wafunge ndoa mwezi Novemba mwaka jana.
Chanzo - Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post