POLISI MOROGORO WAKAMATA WATU 18 TUHUMA KIBAO IKIWEMO ZA WIZI WA SIMU,DAWA,BANGI

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro Willbroad Mutafungwa akionesha simu zilizoibiwa katika mikoa mbalimbali.

Na Jackline Lolah Minja - Malunde 1 blog
Jeshi la polisi mkoani Morogoro limefanikiwa kukamata jumla ya watuhumiwa 18 wa makosa mbalimbali pamoja na vifaa tiba na madawa,simu za mkononi 25, nati 707 za mataruma ya reli ,bangi viroba vinne ,bangi debe 4,bangi kilo 2 bangi puli 6,kete 631 za bangi pamoja na pikipiki aina ya haoujue yenye namba za usajili MC 716CKE ikisafirisha bangi.

Hayo yamesemwa leo Aprili mosi na Kamanda wa polisi mkoani Morogoro Willbroad Mutafungwa alisema watuhumiwa na vifaa hivyo vimekamatwa katika misako mbalimbali iliyofanywa na jeshi la polisi.

"Mnamo tarehe 21 Machi 2020 majira ya saa sita mchana katika kitongoji cha Minjenja wilayani Gairo mkoani Morogoro tulimkamata Daniel Nelson (28) kwa tuhuma za kumtorosha binti mmoja kutoka kwa himaya ya wazazi wake na baada ya kufanyiwa upekuzi alipatikana na vifaa vya matibabu ya binadamu ambavyo anavimiliki bila kibali",ameeleza Kamanda Mutafungwa.

"Mtuhumiwa huwa anatoa huduma za matibabu ya binadamu nyumbani kwake kwa kificho bila kufuata utaratibu na anaendelea kuhojiwa na hatua za kumfikisha mahakamani zinafuata",amesema Kamanda Mutafungwa

Aidha Mutafungwa amesema kuwa tarehe 12 Machi majira ya saa tano asubuhi huko maeneo ya hospitali ya mkoa Morogoro walifanikiwa kumkamata Barnabas Bernad Mayunga (32) mkazi wa Kihonda kwa Mkomola akiwa na madawa mbalimbali ya kutibu binadamu na vifaa tiba bila kibali vikiwa kwenye gari yake yenye namba za usajili T 394 DKP aina ya Toyota Harrier . 

"Mtuhumiwa amekutwa na vifaa tiba pamoja na dawa hayo akimiliki bila kibali lakini uchunguzi wa kina unafanyika kuhusiana na taaluma yake kwa kuwa mtu huyo ameendelea kujitambulisha kama daktari upepelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani",ameeelza.

"Pia mnamo tarehe 15 Machi mwaka huu majira ya saa tisa alasiri askari wakiwa doria na misako walipokea taarifa kuwepo kwa mwanamke Sofia Peter (33) mkazi River side Ubungo Dare s salaam maeneo ya Kingolwira akiwa kwenye bus liitwaloAadvanture likitokea Dodoma kuelekea Dare s salaam akiwa anajaribu kutoroka na simu 25 za aina mbali mbali alizoziiba mikoa ya Mbeya, Iringa na Morogoro. 

“Mtuhumiwa alitumia mbinu ni kwenda studio kupiga picha na kuomba kutafutiwa wasichana wasiopungua 10 ili kuwatumia kwenye tangazo la biashara la sabuni na mafuta na baada ya kuwapata wasichana hao akaondoka nao hadi kwenye maduka ya nguo mjini na kuingia duka moja wapo na kuwataka waanze kujaribu nguo, wakati wakendelea kujaribu nguo hizo akawaomba simu zao ili awapige picha wakiwa wamevaa nguo hizo ndipo alipoondoka nazo akiwaaga kuwa anaingia duka la pili kuangalia nguo nzuri zaidi na kutokomea nazo.  Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa kwa ushirikiano wa polisi mkoa wa mbeya na Iringa na uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani",amesema.

Amesema Pia jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 15 kwa makosa ya kupatikana na kusafirisha bangi na watuhumiwa wote wanahojiwa upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Kamanda Mutafungwa amesema jeshi la polisi linaendelea kutoa wito kwa wananchi wote kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi lapolisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na uhalifu na wanaojihusisha na matukio ya wizi ,usafirishaji, na uuzwaji wa dawa za kulevya kuacha mara moja kwani jeshi lapolisi limejipanga vizuri kudhibiti wizi huo.










Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527