KATIBU MKUU AIPONGEZA MUHIMBILI KUBUNI VAZI LA WATAALAMU KUJIKINGA NA VIRUSI VYA CORONA | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, April 19, 2020

KATIBU MKUU AIPONGEZA MUHIMBILI KUBUNI VAZI LA WATAALAMU KUJIKINGA NA VIRUSI VYA CORONA

  Malunde       Sunday, April 19, 2020
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainab Chaula ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ubunifu wa kushona vazi (PPE) kwa ajili ya Wataalamu wa Afya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona wakati wa kutoa huma kwa wagonjwa.


Dkt. Chaula ametembelea kiwanda kidogo cha kutengeneza mavazi hayo na kuona jinsi yanavyotengenezwa na kuwashauri MNH waendelee kuzalisha mavazi mengi ili kutosheleza mahitaji ya Wataalamu wa hospitali hiyo.

“ Leo nimekuja hapa kuwatia moyo kwa kazi kubwa mnayoifanya. Sisi Kama Serikali tunaichukulia Kama jambo jema hasa kipindi hiki cha mapambano ya COVID-19,” amesema Dkt. Chaula.

Katibu Mkuu, Dkt. Chaula ameiagiza Muhimbili kupeleka vazi Hilo katika mamlaka za kuthibitisha ubora wake ili vazi hilo lianze kutumika rasmi na wataalamu.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Hedwiga Swai amesema ameishukuru Serikali kwa kutambua ubunifu wa mavazi hayo na kwamba wataongeza juhudi kutosheleza mahitaji ya Wataalamu.

Dkt. Swai amesema gharama za kutengeneza vazi moja si kubwa kwani wametumia shilingi 30,000 ukilinganisha na vazi lililothibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambalo moja linagharimu shilingi 350,000.

“ Vazi lililothibitishwa na kupitishwa kutumika na WHO ni shilingi 350,000 hadi shilingi 550,000, inategemea umelinunua kutoka nchi gani, “ amesema Dkt. Swai.

Amesema ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, imewatia moyo kwani ameona jinsi mafundi wanavyotegeneza vazi hilo kwa ustadi wa hali ya juu na hivyo huwezi kuona tofauti kati ya vazi lililothibitishwa na WHO na vazi lililotengenezwa na MNH.

“ Katibu Mkuu ameagiza tumpelekee mavazi manne pamoja na Lile lililothibitishwa na WHO ili apeleke Shirika la Viwango Tanzania (TBS), TMDA na Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili kuthibitishsha Viwango,” amesema Dkt.Swai.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post