PAKA WAAMBUKIZWA CORONA NYUMBANI

Picha ya maktaba ya paka akiwa katika kliniki ya wanyama

Paka wawili wamekutwa na virusi vya corona katika jimbo la New York , wanyama wa kwanza wa kufugwa nchini Marekani kukutwa na maambukizi, maafisa wameeleza.

Wanyama hao ambao wanaishi kwenye maeneo tofauti ya New York , wote walikuwa na dalili za wastani za kushindwa kupumua lakini wanatarajiwa kupona.

Wanasayansi wanafikiri kuwa hakuna uwezekano wa mnyama kumuambukiza binadamu virusi vya corona.

Awali, simba saba na chui katika bustani ya wanyama ya Bronx walikutwa na virusi vya corona.

Idara ya kilimo ya Marekani (USDA) na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC) zilitangaza taarifa kuhusu paka hao siku ya Jumatano.

Mmoja kati ya paka hao alipimwa na kuonesha dalili za homa ya mapafu baada ya mmiliki wake kukutwa na maambukizi.

Mmiliki wa paka wa pili hajapimwa virusi vya corona.

Kumekuwa na idadi ndogo ya wanyama waliotengwa kutokana na kupata maambukizi ya virusi vya corona nchini Marekani.

Hakuna wanyama ambao waliokuwa na maambukizi ya virusi ambao waliumwa sana. Wanasayansi wanafanya uchunguzi kuhusu sababu ya hali hiyo.

Kituo cha kupambana na kudhibiti magonjwa kimesema kuwa wamiliki wa wanyama hawa wa kufugwa nyumbani wawaache wanyama hawa kuchangamana na watu au wanyama wengine nje ya nyumba wanamoishi.
Chanzo- BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527