ZAIDI YA LAINI MILIONI 35 ZASAJILIWA KWA ALAMA ZA VIDOLE


MAMLAKA ya Mawasiliano nchini (TCRA) imesema jumla ya laini 35,813,455 kati ya 43,072,868 zilizounganishwa mitandano zimeshajiliwa kwa alama za vidole mpaka kufikia Machi 10 mwaka huu.

Akizungumza jana wakati wa maazimisho ya Siku ya Haki ya Mlaji Duniani Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba amesema kuwa idadi hiyo ambayo ni sawa na asilimia 83.1 ya laini zote ni wazi kuwa zoezi la usajili wa laini za simu kwa alama za vidole limekuwa na manufaa.

“TCRA mpango wa kusajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole mnamo 2018,zoezi hili limekuwa na manufaa na kupata mwitiko mkubwa ambapo hadi kufikia Machi 10,2020 idadi ya laini zilizounganishwa mitandanoni ni 43,072,868 huku idadi ya laini zilizosajiliwa kwa alama za vidole ni 35,813,455 sawa na asilimia 83.1 ya laini zote,”alisema Mhandisi Kilaba.

Amesema lengo la usajili wa kutumia mfumo huo ni kuimarisha usalama katika matumizi ya simu za mkononi ,kulinda watumiaji na kufanikisha shughuli nyingine za usimamizi.

Amesema wakati watumiaji wakiadhimisha siku ya mlaji ni muhimu wakakumbuka wajibu wa kila mmoja kusajili laini yake ya simu kwa mfumo wa kutumia alama za vidole ambapo kitambulisho kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho ya Taifa nchini(NIDA).

Akizungumzia kuhusu siku ya Haki ya Mteja Duniani Mhandisi Kilaba alisema siku hiyo huadhimishwa kila mwaka Machi 15 kila mwaka ambapo maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu isemayo ‘Mteja Endelevu’.

“Kauli mbiu inajikita katika kusisitiza umuhimu wa upatikanaji wa huduma endelevu nasi katika sekta ya mawasiliano tumekuwa tukilitekeleza hilo,tunalitekeleza na tutaendelea kulitekeleza wakati wote,”alisema Mhandisi Kilaba.

Amesema katika maadhimisho haya TCRA imekuwa ikifanya mikutano mbalimbali na wadau kwa muda wa wiki nzima wakitoa elimu ya mawasiliano katika shule na vyuo mbalimbali katika mikoa ya Shinyanga,Tabora,Arusha,Zanziba na Pwani.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527