Breaking : WAANDISHI WANNE WA HABARI WAUNGUA MOTO MOROGORO | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, March 14, 2020

Breaking : WAANDISHI WANNE WA HABARI WAUNGUA MOTO MOROGORO

  Malunde       Saturday, March 14, 2020


Na Jackline Lolah Minja - Malunde  1 blog
Waandishi wa habari wanne wa Star TV, Global Publishers, Abood Media na Imani Media wameungua baada ya kulipukiwa na mtungi wa gesi, eneo la Mizambarauni Msamvu Morogoro, walipokuwa wakifuatilia taarifa ya moto.Taarifa za awali zinasema waandishi hao wa habari ni Omary Hussein wa Star TV, Salum  Yusuph wa Abood media, Hassan Ninga wa TV Imaan na Nicko wa Global Publishers wamelazwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya matibabu matibabu  na wameungua moto baada ya mtungi wa gesi kulipuka wakati wa uokoaji na wao wakiendelea kupiga picha. 

 Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro (Morogoro Press Club) Nickson Mkilanya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa waandishi hao wa habari wamekumbwa na tukio wakati wakitekeleza majukumu yao.

 "Nimepokea taarifa za ajali ya moto kwa waandishi hawa habari kwa masikitiko, walikuwa wanawajibika na mpaka sasa waandishi wa habari  wawili ambao ni Omary Hussein na Salum bado wapo hospitali wanaendelea na matibabu. Hassan Ninga na Nicko  wameruhusiwa  kutoka",amesema Mkilanya wakati akizungumza na Malunde 1 blog.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema tukio hilo limetokea leo Jumamosi Majira ya saa nane na nusu mchana.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post