WIZARA YA MAJI YATOA TAHADHARI KWA WAMILIKI WA MABWAWA KOTE NCHINI


Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Wizara ya Maji imetoa tahadhari kwa wananchi  wote wakiwemo wamiliki wa mabwawa ya maji  na mabwawa ya tope sumu kuzingatia matangazo  ya utabiri wa hali ya hewa unaotolewa kuhusu mvua za masika za mwaka huu kuwa ni juu ya wastani katika maeneo mengi nchini.



Katika taarifa iliyotolewa na kitengo cha Mawasiliano ,Serikalini kupitia Wizara ya Maji imefafanua kuwa mvua hizo zinaweza kusababisha mabwawa kujaa maji zaidi ya uwezo wake  hivyo kutishia usalama wa wananchi,mali zao na mazingira kwa ujumla.

Taarifa hiyo imesema kuwa mabwawa yanaweza kupasuka kwa sababu ya kujaa  au kutiririsha maji katika mikondo isiyo rasmi [overflow]na miongoni mwa madhara yake ni kuleta mafuriko   katika vijiji,barabara,madaraja na kuharibu miundombinu mingine.

Kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa mwaka huu kuwa na mvua nyingi katika maeneo mbalimbali nchini Wizara imewataka wamiliki wote wa Mabwawa kutekeleza mambo matatu ambayo ni kusafisha utoro wa maji,kudhibiti maji yasisambae katika mazingira pamoja na kuwasilisha mipango ya usalama wa mabwawa na mafuriko kwa mkurugenzi wa Rasilimali za maji ili kukabili dharura itakayotokea   kutokana na mvua za masika  zinazoendelea kunyesha  kama sheria ya Rasilimali za Maji Na.11   ya mwaka 2009 sehemu ya   kumi[x] na kanuni zake za Usalama wa Mabwawa  GN .237  za Mwaka 2013 kifungu cha 16 inavyoelekeza.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527