WIZARA YA AFYA YASEMA UVAAJI HOLELA WA MASK NI HATARI KWA AFYA YAKO


WIZARA ya afya imesema kuwa  kuwa si kila mtu anatakiwa kuvaa kifaa cha kuziba uso ‘mask’ ili kujikinga na homa inayosababishwa na virusi vya corona.

Akitoa maelekezo kuhusu watu wanaotakiwa kuvaa mask, Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Udhibiti na Ufuatiliaji wa Magonjwa Mlipuko, Dk. Janeth Mghaba amesema kifaa hicho kinavaliwa si zaidi ya saa nne tu na mtu ambaye tayari ana maambukizi kusudi asimuambukize mwingine.

Amesema hiyo ni kwa sababu siyo rahisi mtu akakohoa aidha kwa kutumia kiwiko au mkono atakuwa na maji maji na mara nyingi ataweza kumuambukiza mwenzie.

“Kwa hiyo yule ambaye ni mgonjwa tu, tunasema kwamba ukijisikia dalili za kukohoa basi wewe vaa mask yako nenda kwenye kituo cha afya karibu au hospitali.

“Mask pia zinaweza kuvaliwa kwenye sehemu za msongamano au sehemu zenye watu wengi lakini kwa sababu tayari serikali imeshapiga marufuku hii misongamano, hatutegemei kukuona wewe unavaa mask unapita sehemu ambako hakuna msongamano na wewe ni mzima huna maambukizi,” amesema.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527