WABUNGE WA CHADEMA , HALIMA MDEE, ESTHER MATIKO NA ESTER BULAYA WATOKA GEREZANI


Wabunge wa Chadema, Halima Mdee, Esther Matiko na Ester Bulaya wametoka gereza la Segerea leo baada ya kulipa faini ya Sh110 milioni.


Mkurugenzi wa itikadi, uenezi, mawasiliano na mambo ya nje wa Chadema, John Mrema ameendelea kuwashukuru wananchi walio ndani na hata nje ya nchi kwa kujitoa kwao kwa michango mbalimbali iliyosaidia wabunge hao kulipiwa faini zao na hatimaye kutoka gerezani.

Viongozi hawa wa Chadema pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji juzi Jumanne Machi 10, 2020 walihukumiwa kulipa faini ya Sh350 milioni au kwenda jela miezi mitano baada ya kutiwa hatiani kwa makosa 12 kati ya 13 yaliyokuwa yanawakabili.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post