VIRUSI VYA CORONA VYATUA NCHI JIRANI YA RWANDA

Rwanda imethibitisha kisa chake cha kwanza cha virusi vya Corona (COVID-19). Raia wa India aliyewasili nchini humo kutoka Mumbai, India, Machi 8, 2020 amethibitishwa kuwa na virusi vya corona.

Kulingana na wizara ya afya, mgonjwa huyo hakuwa na dalili zozote za virusi vya Corona wakati anawasili nchini Rwanda na alijipeleka mwenyewe kwenye kituo cha afya Machi 13, ambapo alifanyiwa vipimo mara moja.

Kwa sasa anaendelea na matibabu, hali yake imeimarika na ametengwa na wagonjwa wengine. Wote aliokuwa na mgonjwa huyo wanaendelea kutafutwa katika juhudi za kuudhibiti ugonjwa huo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527