BENKI YA TPB YATOA ELIMU KWA WANA AMCOS SHINYANGAMeneja wa TPB tawi la Shinyanga ndugu Jumanne Wagana akizungumza katika mkutano mkuu wa vyama vya Ushirika (AMCOS) Mkoani Shinyanga uliofanyika katika ukumbi wa SHIRECU ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (Tanzania Cooperative Development Commission -TCDC ) Dk. Titus Kamani. 
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Vyama vya Ushirika (AMCOS) Mkoani Shinyanga wakimsikiliza meneja wa Benki ya TPB Ndg. Jumanne Wagana wakati wa mkutano huo.
***
Benki ya TPB imetoa elimu ya kibenki leo Jumamosi Machi 14, 2020 katika mkutano mkuu wa vyama vya Ushirika (AMCOS) Mkoani Shinyanga uliofanyika katika ukumbi wa SHIRECU ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (Tanzania Cooperative Development Commission -TCDC ) Dk. Titus Kamani. 


Katika Mkutano huo Meneja wa TPB tawi la Shinyanga ndugu Jumanne Wagana alitoa elimu kwa wadau wa Ushirika (AMCOS) kuhusu umuhimu wa kutumia benki kama TPB kuweka akiba zao na kupokelea malipo ya Pamba pindi wanapouza mazao hayo.

"Naomba ndugu mtumie benki kutunza na kupokea fedha zenu kwani hii itaondoa upotevu wa pesa lakini inaweka nidhamu katika matumizi ya pesa tofauti na mkulima akipokelea pesa mkononi",alisema Wagana. 

Aidha Wagana aliwakumbusha wana Ushirika wote kuwa kwa Mwaka huu serikali ya Awamu ya Tano imesema watu hawatalipwa pesa mkononi badala yake watalipwa kupitia kwenye benki. 

Alisema akaunti za vikundi vya Ushirika (AMCOS) kwa Benki ya TPB zinafunguliwa bure na hazina makato mwisho wa mwezi kama zilivyo akaunti zingine.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post