Picha : DC MBONEKO AONGOZA MAMIA YA WANAWAKE KUADHIMISHA KONGAMANO LA WANAWAKE 'SHINYANGA WOMEN'S DAY OUT'Kongamano la wanawake Shinyanga mjini (Shinyanga Women's Day Out), lililoandaliwa na Kikundi cha Wanawake na mabadiliko (Women For Change - WFC ), limehudhuriwa na mamia ya wanawake kutoka Shinyanga mjini, kwa ajili ya kupewa elimu mbalimbali ikiwamo ya malezi, afya, sheria, pamoja na jinsi ya kujikwamua kiuchumi.

Kongamano hilo limefanyika leo Machi 7, 2020 kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoa wa Shinyanga, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo, Mboneko aliwataka wanawake Shinyanga mjini washirikiane na kuungana mkono, ikiwamo kwenye masuala ya kuinuana kiuchumi na kuacha tabia ya kutopendana.

Alisema huu ni wakati wa wanawake kushirikiana, kupendana na kuungana mkono kwenye masuala ya kibiashara kwa kununuliana bidhaa, na kuacha tabia kutopendana ili wapate kusonga mbele kiuchumi.

Mkuu huyo wa wilaya alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wanawake kutumia vyombo vya habari na mitandao ya jamii kutangaza shughuli wanazofanya.


“Napongeza sana kikundi hiki cha wanawake na mabadiliko cha Women for Change kwa kufanya Kongamano hili la wanawake Shinyanga mjini, na hasa kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ni Machi 8,2020  kwa kukutanisha wanawake kupewa elimu mbalimbali kwa mstakabali wa maisha yao,”alisema Mboneko.

“Kupitia Kongamano hili naomba wanawake, mpendane, mshirikiane, pamoja na kuungana mkono kwenye biashara mbalimbali ili mjikwamue kiuchumi, ambapo dhana za kuchukiana zilishapitwa na wakati, kipindi hiki ni cha mabadiliko wanawake tuungane na kuwa kitu kimoja,”alisema Mboneko.

"Pia nakipongeza kikundi hiki cha wanawake na mabadiliko kwa kufanya ukarabati wa bweni la wavulana kwenye kituo cha kulea watoto wenye ualbino Buhangija, ili kuwaweka katika mazingira mazuri, mfano ambao unapaswa kuingwa na wadau wengine wa maendeleo",aliongeza Mboneko.

Kwa upande wake Mwenyekiti Msaidizi wa Kikundi cha wanawake na mabadiliko 'Women for Change' - WFC, kutoka Shinyanga mjini Getrude Munuo, alisema kikundi hicho kilianzishwa mwaka 2013 na 2014 walipata usajili, na lengo lao kubwa ni kusaidiana kuinuana kiuchumi pamoja na kufanya shughuli za kijamii.

Alisema wameendesha kongamano hilo kwa lengo la kutoa elimu mbalimbali kwa wanawake wa Shinyanga mjini, ikiwamo ya malezi, afya pamoja na namna ya kushirikiana kibiashara ili kuinuka kiuchumi.

TAZAMA VIDEO WANAWAKE WAKICHEZA MUZIKI

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye Kongamano la wanawake "Shinyanga Women's Day Out" lililoandaliwa na kikundi cha wanawake na mabadiliko Women for Change kutoka Shinyanga mjini leo Jumamosi Machi 7,2020. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye Kongamano la wanawake Shinyanga mjini "Shinyanga Women's Day Out" lililoandaliwa na kikundi cha wanawake na mabadiliko Women for Change kutoka Shinyanga.
Waandaaji wa Kongamano la Shinyanga Women's Day Out wakiwa ukumbini.
Waandaaji wa Kongamano la Shinyanga Women's Day Out wakiwa ukumbini.

Wanawake wakiwa kwenye Kongamano la Shinyanga Women's Day Out.
Meza Kuu 'VIP' wakiwa kwenye Kongamano la Shinyanga Women's Day Out.
Meza Kuu 'VIP' wakiwa kwenye Kongamano la Shinyanga Women's Day Out.

Awali Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiingia kwenye Kongamano la wanawake Shinyanga, " Shinyanga Women's Day Out."

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, wapili kulia, akipiga picha ya pamoja na baadhi ya wanawake na mabadiliko (WCF) wakati alipowasili kwenye Kongamano la wanawake, "Shinyanga Women's Day Out."


Baadhi ya wana kikundi na mabadiliko (WFC) wakipiga picha ya pamoja na wawezeshaji wa mada kwenye Kongamano la wanawake kutoka Jijini Dar es salaam, akiwamo Sadaka Candi ambaye ni mwanasaikolojia (wanne kutoka kulia), akifuatiwa na Mchumi Hilda Kisoka mwenye nguo nyeusi.


Wajumbe wa Kikundi cha wanawake na mabadiliko (WFC), wakifuatilia Kongamano la wanawake ambalo ndiyo waandaaji.

Mwenyekiti Msaidizi wa kikundi cha wanawake na mabadiliko Women for Change Getrude Munuo, akitambulisha wajumbe wa kikundi hicho pamoja na kufungua rasmi Kongamano hilo.


Mwenyekiti wa maandalizi wa Kongamano hilo Fausta Kivambe, akitoa shukrani kwa wanawake kujitokeza kwa wingi kwenye Kongamano hilo la wanawake.


Awali mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwa na mwenyekiti msaidizi wa kikundi cha wanawake na mabadiliko (WFC) Getrude Munuo, wakikata Keki kwa ajili ya kufungua Rasmi Kungamano hilo la wanawake.

Wanawake wa kikundi cha mabadiliko (WFC), Wakifungua Shampeni tayari kwa kuanza kwa Kongamano hilo la Wanawake Shinyanga mjini, "Shinyanga Women's Day Out."

Watoa mada wakiwa wameketi kwenye meza tayari kwa kutoa elimu mbalimbali kwenye Kongamano hilo la wanawake Shinyanga "Women's Day Out."

Mama Edna Shoo akitoa mada kwenye Kongamano hilo la wanawake juu ya Malezi na Mahusiano katika familia.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya akina mama kutoka hospitali ya rufani ya mkoa wa Shinyanga Dk. Rose Malisa, akitoa mada ya Saratani ya Mlango wa kizazi na matiti kwenye Kongamano hilo la wanawake.

Mwanasheria Salome Mbuguni akitoa mada ya Sheria juu ya mirathi pamoja na mwanamke kumiliki mali.
Kongamano linaendelea

Sadaka Candi (Maarufu Ant Sadaka) mshauri wa Saikolojia akitoa mada kwenye Kongamano la  wanawake namna ya kuishi na wanaume pamoja na malezi bora ya watoto katika familia.

Sadaka Candi( Maarufu Anti Sadaka), mshauri wa Saikolojia akitoa mada kwenye Kongamano la wanawake namna ya kuishi na wanaume pamoja na malezi bora ya watoto katika familia.
Mtoa Mada Hilda Kisoka akitoa mada kwenye Kongamano hilo la wanawake namna ya kukua kiuchumi. 
Mbunge wa viti Maalum mkoani Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga akizungumza kwenye Kongamano hilo la wanawake na kuwataka wanawake wapendane.

Wanawake wakiwa kwenye Kongamano la "Shinyanga Women's Day Out" Shinyanga mjini, lililoandaliwa na kikundi cha wanawake na mabadiliko (WFC), wa pili kushoto ni mbunge wa viti maalumu mkoani Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga, na wa kwanza kushoto ni Diwani wa viti maalum manispaa ya Shinyanga Mariamu Nyangaka.

Wanawake wakiendelea na Kongamano la Shinyanga Women's Day Out.

Wanawake wakiendelea na Kongamano la Shinyanga Women's Day Out.

Wanawake wakiendelea na Kongamano la Shinyanga Women's Day Out.

Wanawake wakiendelea na Kongamano la Shinyanga Women's Day Out.

Wanawake wakiendelea na Kongamano la Shinyanga Women's Day Out.

Wanawake wakiendelea na Kongamano la Shinyanga Women's Day Out.

Kongamano la wanawake likiendelea.

Kongamano la wanawake likiendelea.

Kongamano la wanawake likiendelea.

Wanawake wakicheza mziki kwenye Kongamano lao, "Shinyanga Women's Day Out".

Wanawake wakicheza muziki
Wanawake wakiwa kwenye kongamano la Shinyanga Women's Day Out
Wanawake wakiwa kwenye kongamano la Shinyanga Women's Day Out
Wanawake wakiwa kwenye kongamano la Shinyanga Women's Day Out
Wanawake wakiwa kwenye kongamano la Shinyanga Women's Day Out
Wanawake wakiwa kwenye kongamano la Shinyanga Women's Day Out
Wanawake wakiwa kwenye kongamano la Shinyanga Women's Day Out

Awali mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwasili kwenye Kongamano la wanawake "Shinyanga Women's Day Out" kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoa wa Shinyanga, akipokewa na wanawake na mabadiliko (WFC) ambao ndiyo waandaji wa Kongamano hilo.
Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post