SERIKALI YAVUNJA MKATABA ULIOSAINIWA NA KANGI LUGOLA NA WENZAKE

FAUSTINE GIMU 

SERIKALI  imevunja mkataba na Kampuni ya Rom Solution Ltd. ya nchini Romania ulioingiwa baina yake na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa zaidi ya sh.trilioni moja.

Mkataba huo ni ule ulioshtukiwa na Rais John Magufuli kabla hajaingilia kati na kuwatumbua aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola na aliyekuwa Kamishna wa Jeshi la Zimamoto,na Uokoaji  Thobias Andengenye.

Lugola,Andengenyi pamoja na baadhi ya  watumishi wa Jeshi la Zimamoto na Ukoaji walihojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuhusiana na sakata hilo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Jijini hapa,Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene alisema mkataba huo ulivunjwa rasmi Februari 12, mwaka huu.

Waziri Simbachawene amesema Januari 27, mwaka huu wakati wa sherehe za kuapishwa kwake kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Rais alimuagiza kushughulikia suala la mkataba huo tata baina ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Kampuni ya Rom Solutions.

Alisema katika kushughulikia suala hilo, amebaini kuwepo kwa hati ya makubaliano iliyoingiwa Agosti 22, mwaka jana kati ya aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na kampuni hiyo.

“Hata hivyo makubaliano yalikuwa ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya jeshi la zimamoto vyenye thamani ya Euro milioni 408,416,238.16 ambayo kwa fedha za Tanzania ni zadi ya Sh trilioni moja,” alisema Simbachawene.

Amesema serikali baada ya kupitia hati ya makubaliano baina ya aliyekuwa kamishna,  iliona mkataba huo ulikuwa na mapungufu mengi na haikuwa na haja ya kuendelea na makubaliano hayo kwani hayakuwa na tija na hivyo serikali ikaamua kuuvunja Februari 12, mwaka huu.

“Baada ya kupitia hati ya makubaliano baina ya aliyekuwa kamishna,  iliona mkataba huo ulikuwa na mapungufu mengi na haikuwa na haja ya kuendelea na makubaliano hayo kwani hayakuwa na tija na hivyo serikali ikaamua kuuvunja Februari 12, mwaka huu.

Amesema baada ya kuvunjwa kwa makubaliano hayo hakuna hasara wala madai yoyote ambayo serikali inadaiwa kwa sababu mkataba umevunjika na pande zote mbili zimekubaliana.

Alipoulizwa amejipangaje kunusu  mapungufu  yaliyojitokeza   katika Jeshi la Zimamoto na Ukoaji Simbachawene alisema : Mapungufu ya Jeshi la Zimamoto na Ukoaji kama yalivyo kwenye maeneo mengine   hakuna mahala ambako utakuta ‘parfect’ na pamejitosheleza lakini yapo ni ya kawaida na yatashughulikiwa.

“Lakini kwa yale maeneo ambayo tunayahitaji maelekezo Rais alielekeza tutumie kiwanda cha Nyumbu kwa sababu wanauwezo wa kutengeneza magari.

mwisho


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527