HALIMA MDEE, ESTER BULAYA, BONIFACE JACOB WAKAMATWA WAKIJIANDAA KUMTOA MBOWE GEREZANI | MALUNDE 1 BLOG

Friday, March 13, 2020

HALIMA MDEE, ESTER BULAYA, BONIFACE JACOB WAKAMATWA WAKIJIANDAA KUMTOA MBOWE GEREZANI

  Malunde       Friday, March 13, 2020

Wabunge wawili wa Chadema, Halima Mdee na Ester Bulaya, Meya wa Ubungo Boniface Jacob, Katibu wa chama hicho Mkoa wa Dar, Henry Kileo na wanachama wengine wamekamatwa na polisi baada ya kutokea vurugu wakati wakifuatilia Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe  kutolewa katika gereza la Segerea.

Mdee na Bulaya walitoka jela jana baada ya kulipa faini, leo walikwenda kumpokea Mbowe ambaye amekamilisha taratibu za kutoka jela.

Viongozi hao wamekamatwa saa 7:30 mchana baada ya kufika katika gereza hilo na kuanza kuzuiwa na askari wa Jeshi la Magereza waliotumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa chama hicho.

Wakati mabomu hayo yakipigwa, viongozi hao wa Chadema waliwekwa chini ya ulinzi kwa madai ya kukiuka amri halali ya kuwataka kuondoka katika eneo hilo.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post