SERIKALI YA AWAMU YA TANO YAWEZESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA BORA ZA AFYA MKOA WA MOROGORO | MALUNDE 1 BLOG

Monday, March 23, 2020

SERIKALI YA AWAMU YA TANO YAWEZESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA BORA ZA AFYA MKOA WA MOROGORO

  Malunde       Monday, March 23, 2020
Na; Mwandishi Wetu

Shilingi Bilioni 4.5 zimetumika kujenga Hospitali za Wilaya Mkoani Morogoro ikiwa ni jitihada za Serikali kuhakikisha kuwa huduma za afya zinawafikia wananchi wote.

Akizungumza katika kipindi cha ‘TUNATEKELEZA’ Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw.  Loata Ole Sanare amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imewezesha wananchi kufikiwa na huduma bora za fya katika maeneo yao.

“Mkoa wetu kwa sasa una Hospitali za Wilaya katika Wilaya zote baada ya Serikali kutuwezesha kujenga katika Wilaya 3 ambazo hazikuwa na Hospitali za Wilaya”, Alisisitiza Sanare

Akifafanua zaidi, Mhe.  Sanare  amesema kuwa Hospitali hizo zimejengwa katika Wilaya za Malinyi, Morogoro Vijijini na  Gairo  ili kuwezesha wananchi kupata huduma bora za afya. 

Aliongeza kuwa dhamira ya Serikali ya kuwawezesha wananchi kupitia huduma bora imeendelea kutekelezwa kupitia ujenzi wa vituo vya afya na zahanati katika Wilaya zote za mkoa huo hivyo kusogeza huduma kwa wananchi.

Aidha,  Serikali imewezesha Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro mjini kujenga soko lenye thamani ya shilingi Bilioni 18 ili kuimarisha upatikanaji wa huduma  kwa wananchi mjini humo na maeneo ya jirani.

Kipindi cha TUNATEKELEZA kinarushwa kila alhamisi kikishirikisha Wakuu wa Mikoa katika awamu hii ili waweze kueleza utekelezaji katika mikoa yao.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post