RWANDA YATANGAZA MIKAKATI KABAMBE YA KUKABILIANA NA VIRUSI VYA CORONA....MIPAKA YOTE IMEFUNGWA, BAA, KUSAFIRI HOVYO MARUFUKU | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, March 22, 2020

RWANDA YATANGAZA MIKAKATI KABAMBE YA KUKABILIANA NA VIRUSI VYA CORONA....MIPAKA YOTE IMEFUNGWA, BAA, KUSAFIRI HOVYO MARUFUKU

  Malunde       Sunday, March 22, 2020
Wakati ugonjwa wa virusi vya corona  ukiwa unaenea kwa kasi katika maeneo mbalimbali ulimwenguni,Waziri mkuu wa Rwanda Dkt.Ngirente ametoa maagizo 10 ya kukabiliana nao.

Baadhi ya maagizo aliyoyatoa Dkt.Ngirente ni pamoja na kutoruhusu safari zisizo za lazima,malipo ya kieletroniki zaidi yatatumika kuliko kutumia ATM ,Waajiriwa/Watumishi wote wa umma na sekta binafsi watafanya kazi wakiwa majumbani isipokuwa wale watoa huduma muhimu.

Maagizo mengine ni mipaka yote kufungwa,isipokuwa usafiri wa mizigo,safari kati ya miji na wilaya tofauti ndani ya nchi hairuhusiwi isipokuwa kwa sababu za matibabu,usafirishaji wa chakula au bidhaa muhimu zitaruhusiwa.

Pia Dkt.Ngirente ameagiza maduka na masoko yote kufungwa  isipokuwa yale yanayouza chakula,Dawa, vifaa vya usafi huku baa zote zikifungwa.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post