NGULI WA MUZIKI WA AFRO JAZZ MANU DIBANGO AFARIKI DUNIA KWA CORONA

Nyota mkongwe wa muziki wa Afro-jazz Manu Dibango, amefariki dunia leo baada ya kuambukizwa virusi vya vipya corona. 

Wawakilishi wake wamesema mwanamuziki huyo nguli raia wa Cameroon amefariki dunia  leo asubuhi katika hospitali ya eneo la mji wa Paris, Ufaransa. 

Dibango, aliyekuwa na umri wa miaka 86, na anayefahamika kwa kibao cha "Soul Makossa", cha mwaka wa 1972, ni mmoja kati ya nyota wa kwanza wa kimataifa kufariki dunia kutokana na ugonjwa wa COVID-19.

 Ujumbe ulioandikwa kwenye ukurasa wake wa Facebook umesema kuwa mazishi yake yatafanyika kwa usiri mkubwa, na kwamba hafla ya kumbukumbuka itapangwa katika wakati muafaka.

 Dibango alitengeneza muziki wa Afro jazz na pia kuuchanganya na muziki wa kitamaduni wa Cameroon.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527