RAIS WA GUINEA-BISSAU ATANGAZA KUJIUZULU BAADA YA KUKAA SIKU MOJA TU MADARAKANI


Cipriano Cassama, Rais aliyetawazwa kama rais wa mpito wa Guinea-Bissau siku ya Ijumaa jioni, ametangaza kwamba anajiuzulu wadhifa wake baada ya kukaa madarakani kwa siku moja, akisema maisha yake yalikuwa hatarini.


Cipriano Cassamá alichaguliwa na wabunge kuwa rais baada ya chaguzi zilizosusiwa mwezi mwezi Desemba. 


Hatua hii ni pamoja na ukweli kuwa Jenerali wa jeshi wa zamani Umaro Cissoko Embaló tayari alikwisha apishwa kuwa rais katika hoteli mji mkuu wa nchi hiyo, Bissau

Katika taarifa fupi aliyoitoa akiwa nyumbani kwake huko Bissau, akilindwa na askari wa ECOMIB, kikosi cha askari wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika ya Magharibi, ECOWAS, na baadhi ya askari wa Guinea, Cipriano Cassama amesema "usalama wangu uko hatarini". Amebaini kwamba Jumamosi jioni, kuna askari walikuja kuwatafuta walinzi wake. Amesema ana hofia usalama wake na wa familia yake.

Amesema pia anataka kuepusha "mapigano kwa maslahi ya taifa na raia wa Guinea-Bissau" na kulaani kitendo cha jeshi kushikilia kwa nguvu makao makuu ya Bunge la taifa.

Cipriano Cassama alitawazwa bungeni siku ya Ijumaa jioni na wabunge 52, hasa kutoka chama cha PAIGC. Kabla ya hotuba yake, Teodora Gomes, mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kihistoria, alimwomba asiachie ngazi na asitoe tangazo hilo la kujiuzulu, lakini ameamua kujiuzulu, mashahidi wanasema.

"Nikiangalia vitisho vya kifo vilivyotolewa dhidi yangu, dhidi ya walinzi wangu, naona kwamba usalama wangu uko hatarini. Nimeamua kuchukua uamuzi huu, kuzuia makabiliano kati ya vikosi kutoka upande wa pili na vikosi ambavyo vinanilinda na pia kuzuia vita, sijui kama naweza kuviita vita vya kiraia au umwagaji damu, " amesema Cipriano Cassama.

"Kwa hivyo nchi yetu inakabiliwa na mgogoro mpya wa baada ya uchaguzi, mgogoro ambao bado haujatatuliwa kati ya wagombea wawili, Umaro Sissoco Embalo na mpinzani wake, Domingos Simões Pereira, ili tuweze kujua mshindi halali", ameongeza Bw. Cipriano.

Guinea-Bissau imekutwa na matukio tisa ya mapinduzi tangu mwaka 1980.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post