NHIF TANGA YATUA KILINDI KUHAMASISHA WANANCHI JUU YA VIFURUSHI VIPYA

< div class="separator" style="clear: both; text-align: center;">  MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akizungumza na waumini wa kanisa la Adventist (Wasabato) wakati akihamasisha juu ya vifurusi vipya vya mfuko huo katika halmashauri ya wilaya ya Kilindi mkoani Tanga
  MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akitoa elimu kwa mfanyabiashara wa viatu wilayani Kilindi kuhusu umuhimu wa kujiunga na bima ya afya wakati wa uhamasishaji wananchi juu ya vifurushi vipya katika halmashauri ya wilaya hiyo.
 AFISA Metekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Macrina Clemence  kulia akiwa na Mhasibu Mwandamizi wa NHIF Tanga Fredrick Mtangoo wakihamasisha mpango wa bima ya afya kwa wakazi wa mji wa Songe wilaya ya Kilindi wakati uhamasishaji wananchi juu ya vifurushi vipya katika halmashauri ya wilaya hiyo.

 AFISA Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Tanga Josephine John akitoa elimu kwa wananchi wa mji wa Songe wilaya ya Kilindi wakati uhamasishaji wananchi juu ya vifurushi vipya katika halmashauri ya wilaya hiyo.
 AFISA Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Tanga Josephine John akitoa elimu kwa wananchi wa mji wa Songe wilaya ya Kilindi wakati uhamasishaji wananchi juu ya vifurushi vipya katika halmashauri ya wilaya hiyo.

 AFISA Metekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Macrina Clemence kulia akitoa elimu kwa wafanyabiashara wa soko la Songe wilayani Kilindi  juu ya vifurushi vipya katika halmashauri ya wilaya hiyo.
 AFISA Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Tanga Josephine John kushoto akitoa elimu kwa mfanyabiashara kwenye mji wa Songe wilaya ya Kilindi

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) umepiga kambi wilayani Kilindi Mkoani Tanga kwa ajili ya zoezi la uhamasishaji wananchi juu ya vifurushi vipya katika halmashauri ya wilaya hiyo.


Uhamasihaji huo ulifanyika kwenye maeneo  makao makuu ya  wilayani hiyo Songwe kwenye maeneo ya kanisani, msikitini,sokoni ,vituo vya bodaboda na stendi ya mabasi lengo kubwa kuwapa uelewa wananchi umuhimu wa kujiunga na mfuko huo.


Akizungumza wakati wa uhamasishaji huo Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu alisema kwamba lengo la kufika wilayani humo ni kuwafikia wananchi na kuzungumza nao juu ya umuhimu wa mfuko huo.


Alisema kwamba wananchi wengi,wafanyabiashara ndogondogo ,wananchi wa kawaida  walifikiria bima ya Afya ni kwa ajili ya viongozi,wakubwa na waajiriwa lakini wao wamefika kuwaeleza kwamba mfuko huo ni kwa ajili ya wananchi wote.


Meneja huyo alisema kwamba hivi sasa wana fao la Jipimie ambalo wamefika wilayani humo kuzungumza na wananchi katika maeneo yao ya biashara kuhusu umuhimu wa kujiunga nao.


“Kubwa zaidi wafanyabiashara wanapaswa kutambua kwamba ili waweze kuendeela na biashara zao ni muhimu kuwa na bima ya afya watatibiwa wakati wanapoumwa na hawatamaliza mitaji yao kwa sababu gharama za matibabu hazitawasumbua “Alisema Meneja huyo .


Aidha alisema pia alisema familia wakati mwengine zimekuwa zikiingia kwenye matitizo wakati mtoto anapoungua,mama hivyo ni fursa nzuri ya wananchi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanajiunga na bima ya afya ili waweze kunufaika na matibabu wakati wanapougua.


Akizungumzia mpango huo,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilindi Bakari Kingalangala alisema kwamba mpango wa bima ya afya ni muhimu sana kwa jamii kwa sababu watu ambao hawana bima ya afya wanapoungua wanatoa fedha nyingi sana kugharamia matibabu na wakati mwengine kuyumba kiuchumi.


Alisema lakini wanapokuwa na bima ya afya inawasaidia kuweza kupata matibabu bila kuwaza kwamba watapata wapi fedha za kwenda kupata matibabu wanapoungua.


“Bima ya Afya ni muhimu sana kwa jamii kwa sababu mimi mwenyewe nimewaona watu ambao hawana uwezo wakipata mateso wakifika vituo vya afya, hospitalini kama huna bima unatoa fedha nyingi sana lakini ukiwa nayo inakusaidia kutibiwa na unaepuka gharama kubwa”Alisema.


Mwenyekiti huyo alisema kwamba  wayakuwa wahamasishaji kuwaeleza viongozi wa chama ngazi ya wilaya, kata  na vijiji umuhimu wa kujiunga na mpango wa bima ya afya ili kuweza kunufaika na huduma za matibabu pindi wanapougua.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post