MWANAMFALME CHARLES APATA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA


Mtoto wa Malkia Elizabeth, Mwanamfalme Charles (71) amepata maambukizi ya COVID19, Mke wake aitwaye Camilla (72) ‘Duchess of Cornwall’ amepimwa na kuthibitika hana maambukizi.

Kwa mujibu wa taarifa, Mwanamfalme alionesha baadhi ya dalili za Virusi hivyo Jumapili. Vipimo vilichukuliwa siku inayofuata na leo vimethibitisha kuwa ana maambukizi ya CoronaVirus.

Haijafahamika ni wapi Mwanamfalme Charles amepata maambukizi hayo lakini amekuwa akikutana na watu mbalimbali katika wiki zilizopita, kama sehemu ya majukumu yake.

Taarifa iliyotolewa imesema anaendelea vizuri na yupo karantini nyumbani huko Scotland huku akiendelea na kazi zake.

Alikutana na Malkia Elizabeth kwa mara ya mwisho Machi 12 na imeelezwa kuwa afya ya Malkia huyo ni nzuri.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post