MKE WA WAZIRI MKUU WA CANADA JUSTIN TRUDEAU AKUTWA NA VIRUSI VYA CORONA


Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau na mke wake watabaki kwenye karantini kwa siku 14 , baada ya mkewe Sophie Gregoire Trudeau kukutwa na virusi vya corona.

Sophie Gregoire Trudeau ''anaendelea vizuri na dalili alizonazo si mbaya'' alisema mkurugenzi wa mawasiliano wa Waziri Mkuu.

Bwana Trudeau pia atakuwa kwenye karantini kama hatua ya tahadhari. Hatapimwa katika hatua za sasa kwa kuwa haoneshi dalili za maambukizi.

"Waziri Mkuu yuko katika afya njema na hana dalili zozote za maambukizi. Hata hivyo, kwa tahadhari na kulingana na ushauri wa madaktari, atawekwa


Waziri Mkuu wa Canada aliwapigia simuwenzake wa Italia, Marekani na Uingereza Alhamisi mchana, ofisi yake imesema. Siku ya Ijumaa, atakutana na wasaidizi wake kutoka mikoa yote ya Canada ili kujadili jinsi gani ya kupambana dhidi ya ugonjwa wa Covid-19, ambao umeshika kasi nchini Canada katika siku za hivi karibuni.

Zaidi ya kesi 150 ziliripotiwa nchini Canada Alhamisi wiki hii, hasa katika Jimbo la Ontario, katikati mwa nchi, na katika eneo la Magharibi, ambapo mtu mmoja alifariki dunia baada ya kuambukizwa virusi vya ugonjwa huo. karantini kwa muda wa siku 14, "kimesema chanzo hicho


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527