MAREKANI YAFANYA MASHAMBULIZI YA KULIPIZA KISASI DHIDI YA WANAMGAMBO WA IRAN


Marekani imefanya mfululizo wa mashambulizi ya anga dhidi ya maeneo ya wanamgambo wa Kishia wanaoungwa mkono na Iran nchini Iraq.

Wanamgambo hao wanaaminika kuhusika na shambulio la roketi siku moja kabla, ambalo liliwaua askari wawili wa Marekani na mmoja wa Uingereza kwenye kambi moja iliyoko kaskazini mwa Baghadad. 

Taarifa iliyotolewa na wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon, imesema mashambulizi hayo yameyalenga maeneo matano yanayohifadhi silaha, yakitumiwa na wanamgambo wa Kataib Hezbollah ndani ya Iraq. 

Waziri wa ulinzi wa Marekani Mark Esper, ameonya kuwa wamejiandaa kuchukua hatua zozote muhimu ili kuvilinda vikosi vyake nchini Iraq na ukanda mzima. 

Rais Donald Trump aliidhinisha kwa haraka mashambulizi hayo ikiwa ni hatua ya kujibu shambulio la Jumatano kwenye kambi ya jeshi ya Taji mjini Baghdad. 

 -DW


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527