MGONJWA WA KWANZA WA VIRUSI VYA CORONA AWAOMBA MSAMAHA WATANZANIA


Mtanzania wa kwanza kuthibitika kuwa na ugonjwa hatari unaosababishwa na Virusi vya Corona, anayejulikana kwa jina la Isabella Mwampamba, amezungumza leo kwa njia ya simu na kuwataka watanzania wasiwe na hofu na kikubwa wazidi kuchukua tahadhari ya ugonjwa huo.



Akizungumza leo Jumatano Machi 18, 2020 kwa njia ya simu katika mkutano wa wanahabari ulioandaliwa na Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu uliofanyika katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Arusha,  Mrisho Gambo amesema, “ninaendelea vizuri, namshukuru Mungu kwa kunilinda nawaomba msahama watanzania kwa maana kuwa mgonjwa wa kwanza kuugua corona iliyoleta  taharuki nchi nzima na watu wengi wanaona kwamba mimi ni kisababishi."

Isabela amesema kwa sasa hana dalili zozote za ugonjwa huo na kwamba hana homa wala mafua.



Aidha, Waziri Mwalimu amesema mtandao wa watu 26 walioshirikiana na mgonjwa huyo wako chini ya uangalizi na vipimo vya sampuli vimeshapelekwa jijini Dar Es Salaam na majibu yatatolewa wakati wowote kuanzia sasa.

Machi 16, 2020, Tanzania ilithibitisha kisa cha kwanza cha mgonjwa wa Corona, aliyetokea nchini Ubelgiji na kutua katika Uwanja wa Ndege wa KIA.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527