MEYA MANISPAA YA IRINGA ANG'OLEWA MADARAKANI


Baraza la Madiwani la Manispaa ya Iringa limemwondoa Meya wa Manispaa ya iringa-Chadema Alex Kimbe baada ya kupiga kura ya kutokuwa na imani nae kufuatia tuhuma mbalimbali za matumizi mabaya ya madaraka.

Kimbe ambaye anatokana na chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema ameng’olewa madarakani leo Jumamosi Machi 28, 2020 katika kikao maalum cha madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo.

Akitangaza matokeo ya kura zilizopigwa, mwenyekiti wa kikao ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa, Joseph Ryata amesema wajumbe waliohudhuria kikao ni 26 na kura 14 zimeridhia kumuondoa meya huyo.

Miongoni mwa tuhuma ambazo alikuwa anakabiliwa nazo Kimbe ni matumizi mabaya ya madaraka ikiwamo kufanya uamuzi bila kuzingatia kanuni za kudumu za Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527