MBABE WA ZAMANI WA KIVITA DRC GERMAIN KATANGA AACHIWA HURU | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, March 18, 2020

MBABE WA ZAMANI WA KIVITA DRC GERMAIN KATANGA AACHIWA HURU

  Malunde       Wednesday, March 18, 2020

Kiongozi wa zamani wa kundi la waasi katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Germain Katanga, aliyekuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 12 katika mahakama ya kimataifa ICC, ameachiliwa huru.

Hatua hii ya kumwacha huru Germain Katanga inakuja siku moja baada ya kuachwa huru kwa kiongozi mwingine wa waasi wa UPC Thomas Lubanga jijini Kinshasa nchini humo.

Taarifa ya kuachwa kwake huru imetolewa hapo jana na mpwa wake Jeannot Malivo Kagaba huko Kinshasa na kuthibitishwa mkuu wa shirika lisilokuwa la kiserikali linalotetea haki za wafungwa, Emmanuel Cole, na ambaye aliiambia AFP kuwa ni baada ya kukamilishwa kwa hatua zote za kisheria.

Katanga mwenye umri wa miaka 43, alihukumiwa kifungo cha miaka 12 Mwaka 2014 kwa kosa la kudhibiti uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika shambulio la kijiji huko Ituri, alihusika katika mauaji ya watu takriban 200 mnamo mwaka 2003 kaskazini mashariki mwa DRC.

-RFI


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post