MAREKANI YAFUATA NYAYO ZA ULAYA KUKABILIANA NA VIRUSI VYA CORONA


Marekani imechukua hatua kadhaa za kukabiliana na kusambaa kwa ugonjwa hatari wa Covid-19, ambao Shirika la Afya Duniani, WHO, liliutangaza kuwa janga la kimataifa.

Mikusanyiko ya watu kumi ndiyo imeruhusiwa nchini Marekani, sheria ya kutotoka nje usiku imetangazwa katika Jimbo la New Jersey. Pia hatua kadhaa zimechukuliwa kwa maeneo ya miji kama New York, Chicago na Los Angeles.

Marekani inafuata nyayo za nchi kadhaa za Ulaya kwa kuchukua hatua kali kwa kukabiliana dhidi ya ugonjwa hatari wa Covid-19.

Rais Donald Trump ambaye Jumapili Machi 15 alipiga marufuku mikusanyiko ya watu zaidi ya hamsini, ameamua kubadili marufuku yake hiyo Jumatatu wiki hii kwa kuweka marufuku kwa mikusanyiko ya watu zaidi ya kumi.

Hatua nyingine zilizochukuliwa, ni pamoja na shule, baa, migahawa kufungwa, kuepuka safari zisizo za muhimu.

Hatua hizi zilitangawa kupitia njia ya vidio katika mkutano na wakuu wa majimbo ya Marekani.

"Kuna wimbi la hatua zilizochukuliwa nchini kote - ni hatari," amesema Gavana wa Jimbo la New York, Andrew Cuomo, ambaye ni mpinzani wa kisiasa wa rais Trump.

Wakati kesi za maambukizi zilizothibitishwa nchini Marekani zinakaribia watu 4,300 - ikiwa ni pamoja na vifo zaidi ya 74 - New Jimbo la Jersey, jirani na New York, pia ni jimbo la kwanza nchini Marekani kutangaza Jumatatu wiki hii sheria ya kutotoka nje usiku (baada ya eneo la Porto Rico).


-RFI


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post