KOREA KASKAZINI YAFYATUA MAKOMBORA MENGINE MAWILI

Korea Kaskazini  leo imefyatua makombora mengine mawili kuelekea baharini.


Vyombo vya habari kutoka Korea Kusini vimeinukuu wizara ya ulinzi ya nchi hiyo ikitangaza kuwa, makombora hayo mawili yamefyatuliwa mapema leo katika mji wa Korea Kaskazini wa Wonsan kuelekea baharini.

Tarehe mosi Januari, Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alitangaza kuwa, miradi ya nyuklia na majaribio ya makombora ya nchi yake yataanza tena endapo mazungumzo ya nchi hiyo na Marekani hayatoanza tena.

Mazungumzo kati ya Marekani na Korea Kaskazini hivi sasa yameingia kwenye mkwamo baada ya kuvunjika mazungumzo kati ya pande hizo mbili yaliyofanyika Hanoi, Vietnam mnamo mwezi Februari mwaka 2019.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527