KAMPUNI ZA MAWASILIANO YA SIMU ZINAVYOSAIDIA KUINUA WANAWAKE NCHINI TANZANIA


Wiki iliyopita wanawake barani Afrika walisherehekea Siku ya Kimataifa ya Mwanamke. Siku hii muhimu husherehekea mafanikio ya mwanamke kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa na kuchagiza mjadala wa usawa wa kijinsia.  

Nchini Tanzania usawa wa kijinsia umeongezeka katika miaka ya karibuni kutokana na nguvu za serikali, taasisi na watu binafsi kuweka mazingira ya upatikanaji wa elimu kwa mtoto wa kike na haki ya mwanamke kumiliki na kutumia ardhi.Licha ya maendeleo hayo, yapo mengi ambayo inabidi kufanywa kuendelea kumpa nafasi zaidi mtoto wa kike. 

Eneo mojawapo ambalo kuna mengi ya kufanya ni katika teknolojia na mawasiliano. Takwimu na hivi karibuni zinaonyesha katika suala la umiliki wa simu za mkononi Tanzania kuna pengo la asimili 9 kati ya wanawake na wanaume, wanaume wakiwa juu. 

Takwimu zinaonyesha pia kwamba hata katika upatikanaji wa mtandao wa intaneti, wanaume wako juu zaidi kwani kuna pengo la asilimia 13 kati ya wanaume wenye uwezo wa kupata na kutumia intaneti ukilinganisha na idadi ya kundi hilo upande wa wanawake. 

Sote tunafahamu kwamba mtandao wa intaneti ni moja ya njia bora za kuinua aina ya maisha ambayo mtu anaishi. Mfano, intaneti inatoa nafasi ya kupata huduma za fedha, bima za afya na hata nafasi za kazi. Hii leo, mtandao wa intaneti na kuunganishwa kidijitali kunawapa nafasi wanawake ambao zamani hawakuwa na fursa nyingi, fursa mpya ya kufaidi hayo yote.  


Bahati nzuri, hapa Tanzania sekta ya mawasiliano ya simu imeleta namna mpya na za kibunifu kupata faida za kuuganisha kidijitali kwa wanawake.


 Kampuni kama Tigo imeunda apps zinazosaidia wanawake kuendesha na kusimamia mipango yao ya fedha. Mfano Tigo Pesa App inawapa wanawake nafasi kuweka fedha, kufanya malipo na hata kupata mikopo.

 Mbali na hiyo, Tigo pia inasaidia kuhakikisha kwamba wanawake wanapata ujuzi ili kufurahia fursa hizi. Katika hili, Tigo Tanzania wamezindua programu kama “Apps and Girls” ambapo wanawafunzi wa kike wanafundishwa mbinu za kuvuna fursa katika dunia ya kidijitali. 


Katika haya yote, lazima kukumbuka kuwa programu kama hizi za kampuni za simu zimewezekana kutokana na miaka mingi ya uwekezaji wa kampuni hizi. Uwekezaji huo umejenga msingi wa mipango kama hii ambayo inawapa nguvu na kuwainua wanawake pamoja na jamii kwa ujumla. Ili kuhakikisha kwamba kampuni hizi zinaendelea na mipango ya namna lazima taifa letu liendee kuunga mkono ukuaji wa sekta hiyo kwa kuipa mazingira bora ya uwekezaji na sheria bora za kiuendeshaji. 

Tuendelee kufanya kazi pamoja kuunga mkono mipango kuwainua watoto wa kike na wanawake kwa ujumla.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post