KAMATI YA BUNGE YATAKA BAJETI MAENDELEO YA JAMII TENGERU


Na Mwandishi Wetu Arusha
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imeitaka Serikali kuongeza na kutoa fedha za miradi ya maendeleo ya jamii katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini.


Akitoa maelekezo kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inayosimamia Taasisi ya Maendeleo ya Jamii leo tarehe 16/03/2020 mkoani Arusha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba ametaka kupelekwa kwa bajeti ya maendeleo katika katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru na vyuo vya Maendeleo ya Jamii ili kuweza kutekelza miradi ya maendeleo.

Ameongeza kuwa kada ya Maendeleo ya Jamii ni muhimu kwa maendeleo ya jamii yetu hivyo nguvu kubwa inahitajika katika kuwekeza katika Taasisi na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii ili kuweza kupata wataalam wa Maendeleo ya Jamii watakaoleta mabadiliko katika taifa.

" Hili sio suala la kawaida Taasisi na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kujitoa na kufanya kazi huku wakiwa hawana bajeti ya maendeleo, wapeni Bajeti wafanye makubwa" alisema

Amesisitiza uongozi wa Wizara Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii kusimamia Taasisi na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii chini ya Wizara ili viweze kuwa na tija kwa maendeleo ya taifa kwa kuzalisha wataalam watakaosidia kuleta mabadiliko katika jamii.

Akitoa taarifa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru imeweza kufanya ukatabati na ujenzi wa majengo mbalimbali ikiwemo Maktaba ya kisasa yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi...


Ameongeza kuwa Taasisi imejipanga katika kutatua changamoto zilizopo ikiwemo kutenga fedha za ndani zitakazosaidia kuondokanan changamoto za kimiundo mbinu na utawala.

"Tumekuwa na changamoto nyingi za kimiundo mbinu katika Taasisi yetu na tumejipanga kwa kutenga fedha za ndani ili kusaidia kuondokana na changamoto zinazotukabili" alisema

Amesema kuwa Taasisi imeanzisha vituo muhimu katika maendeleo ya nchi ikiwemo Kituo cha kidijitali chenye lengo la kuandaa mawazo na kuzalisha miradi mbalimbali kwa wanafunzi na wananchi ili kuwawezesha kiuchumi na kituo cha machapisho ya wanawake kinacholenga kutoa fursa mbalimbali za kiuchumi hasa kwa wanawake.

Mmoja wa mnufaika wa Kituo cha kidijitali cha Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kutoka Kitomary HotCulture Project Bw. Joshua Kitomari amesema kituo hicho kimemsaidia kuanziasha biashara kulima maharage mabichi na ameweza kuajiri wafanyakazi wa kudumu kumi na wafanyakazi wa muda100.

"Kituo cha Kidijitali kimeniwezesha nilijidunduliza katika mkopo nilopata wa masomo na kuwekeza katika kilimo na niliwekeza shillingi Millioni moja na inanipafaidabya shillingi Millioni mbili" alisema

Akichangia Mjumbe wa Kamati hiyo na Mbunge wa Jimbo Hawa Ghasia ameishauri Taasisi kuzidi kuwekeza zaidi katika Taasisi iliyopo Tengeru kuliko kuwaza kuanzisha matawi ya Taasisi hiyo katika mikoa mingine.

"Niwapongeza kwa kuzingatia masuala ya kijinsia katika utendaji kazi wa Taasisi ambapo wanawake wamepewa nafasi sawa na wanaume katika utekelwzaji wa majukumu ya Taasisi" alisema

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imetembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru iliyopo chini ya Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post